Sunday, November 4, 2007

TSPCA yapinga wanyama kuuawa

Ddc

Na Mobini Sarya

HATIMAYE Shirika la Maendeleo Mkoa wa Dar es salaam,(DDC) limetoa taarifa kuwa Mkandarasi aliyekuwa anajenga vibanda vya biashara eneo la DDC Kariakoo anamkataba unaomwezesha kujenga na kupangisha (BOT).

Taarifa hiyo inaonekana kuhitimisha mvutano uliokuwa unaendelea chinichini kuhusu ni nani anaeyestahili kupangisha na kuendesha eneo hilo lenye vibanda 64, kati ya Mkandarasi ambaye ni Kampuni ya ujenzi Nimeta Construction iliyojenga na Shirika la DDC.

Kampuni ya Nimeta ilipewa Tenda ya ujenzi huo ulionza Mei Mwaka huu baada ya wafanyabiashara 52 kuoondolewa hapo kwa maelezo kuwa eneo baada ya ujenzi kukamilika watalejeshwa hatua ambayo walipinga na kufikia hatua ya kuchangishana pesa ili wajenge wenyewe wakidai kuwa mkandarasi akijenga atawanyima nafasi ya biashara.

Akizungumza na Tanzania Daima Mwishoni Mwaka wiki Meneja Utumishi wa DDC, Shabani Juma alisema kuwa kasasa vibanda hivyo vimekwishakamilika wanachosubiri, mkandarasi huyo atangaze tenda kwenye vyombo vya habari ili anayehotaji aombe.

Maelezo hayo yanapingana na maelezo ya awali yaliyokuwa yanatolewa na Meneja wa Shirika hilo Mhando Muya alipokua akielezea ujenzi wa Vibanda hivyo na yanakuwa kama pigo kwa wale wafanyabiashara walioondolewa hapo kwani inavyoonekana Mkataba wa BOT utakuwa unampa uwezo mwekezaji kupangisha mpangaji anayemtaka yeye.

Ingawa Mhando mara zote amekuwa akisisitiza kuwa mkandarasi anajenga tu nakujiondoa wao wanawapangisha, wakiwapa kipaumbele wafanyabiashara walioondolewa, hata hivyo baada ya taarifa hiyo kutolewa hakuweza kupatika mara moja kuelezea upi upi msimamo wapamoja kuhusiana.

na Mobini Sarya

manispaa ya Ilala yakubali umbwa wote wachanjwe bure

MANISPAA ya Ilala imekubali ombi la Chama cha kuzuia ukatili kwa wanyama (TSPCA), ambacho kilimwadikia barua Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kikiomba asitishe zoezi la kuwasaka na kuwaua wanyama wanaofungwa ambao watabainika wakizurura mitaani bila kuwa na chanjo chanjo ya kichaa.

Akizungumza na Tanzania Daima Ofisini kwake katibu mtendaji wa chama hicho, Johari Gessan alisema kuwa baada ya kukubaliwa sasa wataanza kama awali manispaa hiyo ilikuwa ikisimamia zoezi la chanjo kwa umakini baada ya hapo watapita nyumba kwa nyumba kuwachanja wanyama wote.
Pia Gessan amesema zoezi hilo ambalo litaanza jumatatu watakuwa wanagawa cheni kwa wamiliki wa wanyama hao kuwafungia wanyama hao wasizurure, kwa wanyama ambao watabainika hawana mmilki watawakamata na kuwafundisha tabia njema na kumpa mtu yeyote atakayetaka huku waakimjengea kibanda bure.
“Baada ya ombi letu kukubaliwa tutaanza jumatau kupita nyumba kwa nyuma kuwahamasisha watu wajitokeze kuchanja wanyama wao, tutashirikiana na maaafisa mifugo wa kata, zoezi litakaloenda sambamba na kugwa cheni pamoja na kuwahesabau wanyama wote”alisema Gessan.
Katika barua waliyokuwa wamemwandikia mkurugenzi wa manispaa hiyo ilikuwa inanukuu tangazo lililotolewa Oktoba 10 mwaka huu lililokuwa likitaarifu kuwapo kwa msako wa kuwaua mbwa, paka na nyani ambao hawajapata chanjo za kichaa.
Gessan, alisema badala yake kinatoa pendekezo la kufanya kampeni za muda mrefu na za kudumu kwa wananchi wote kuhusu utunzaji wa mifugo na kuwepo kwa huduma zao za msingi, kazi ambayo tayari wamekwishaianza katika ngazi ya kata na serikali na serikali za mitaa wakianzia na Mkoa wa Dar es Salaam.
TSPCA kimeomba wananchi kutoa taarifa pale wanapoona wanyama wanateswa na kunyanyaswa bila sababu ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria kwani ni wanaharakati pekee wanaotetea haki za wanyama kisheria.



juu

No comments: