Monday, October 29, 2007

Alichokisema butiku kwa upanambele ya waandishi wa habari maelezo

Butiku
NA m S

WIKI iliyopita Mwanasiasa Mkongwe wa Chama Chama Mapinduzi CCM, Joseph Butiku ambaye pia alikuwa msaidizi wa Karibu wa Rais wa Kwanza Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarag Nyerere, alijtokeza mbele ya waandishi wa habari na kusema maneno makuu yanayoashiria mstakabali w a taifa hili.

Ni kiwa miongoni mwa waandishi tuliohudhuria kikao hicho ukumbi wa idara ya habari MAELEZO nimeona ni vema nikaandika kwa kina aliochokuwa anakilenga katika mazungumzo yake, wakati alipoanza kujitambulisha kama Raia Mwaminifu na Mwanachama mwanzilishi wa CCM aliyejitokeza bila kutumwa na Tasisi ya Mwalimu Nyerere “sikuja kama nimetumwa na mfuko hapana nimekuja kama mimi” alisema.

Aliendelea ‘mimi ni bubu huwa sipendi kusema maneno haya nah ii ni kutokana na jinsi tulivyolelelewa kimaadili, leo nimeamua kusema kutokana na ujmbe unaotolewa kwenye vyombo vya habari ambao unahusu viongozi,sisemi kwa ushabiki au kama au kama mpinzani au mtu asiye na adabu nayasema haya kwa dhati kabisa na pale ninapo taja majina sio kama mpuuzi ila nazingatia maadili ya uongozi.

Mwanasiasa huyo alisema kuwa ameamua kujitokeza baada ya kuona kelele za rushwa zinazidi kuwa nyingi, usimamizi mbovu wa maliasili zetu ,umasikini kuzidi kuongezeka ,mali zina potea hovyo na wanaopiga kelele ni sisi wenyewe watanzania.

“kelele hizo zinahusu viongozi na uongozi wan chi, sisi sote kila mmoja anakichwa kinachomuongoza kwa hiyo wote ni viongozi ,matatizo haya yanayoizungumzwa ni yetu sote” Alisema huku akionyesha Katiba ya kwanza iliyoandikwa wakati wa uhuru na iliyotambua kuwepo serikali ya Muungano wa Tanzania katika hiyo ilikuwa na mambo manne ya aliyoyasoma ambayo ni;vyombo vyote vya kiserikali lazima vieleweke kwa wananchi ,Mamlaka inayoongoza itoshe katika kusimamia shughuli, Bunge lijitegemee na mwisho alisema lazima utawala wa kisheria ukubaliwe.

Na ndivyo inapaswa kutendwa hata Rais anaapa kuilinda katiba anapochaguliwa pia anaapa kuwa ataongoza bila upendeleo wowote ikiwemo kuwapendelea ndugu zake na kwa upande wa chama chama cha Mapinduzi katiba inasema hvyo ,hizi katiba zote mbili zinatupa uhuru wa kushughulika na mambo yetu kwa mjibu wa katiba.

Butiku anakumbusha kuwa wakati wachama kimoja kiongozi alikuwa anaapa kuwa hatapokea wala kutoa rushwa leo imepita zaidi ya miaka 40 tangu iandikwe katiba ya mwaka 1962 iliyoasisiwa na Mwalimu Nyerere ,Maadili yameporomoka na Rushwa hapa nchini sasa imekuwa kama ugonjwa wa UKIMWI usio na tiba wakati katiba zote zinazuia.

Anasema kuwa Rushwa ipo kwa sababu viongozi wakuu hawasimamii ipasavyo maadili ipasavyo ,wangeyafuata na kuheshimu katiba ya nchi na chama haya yote yanayozungumzwa na kupigiwa kelele yasingetokea hivi sasa.

Kwa mtazamo wake anaona Suala la Rushwa linachakigiwa kwa kiasi kikubwa na wananchi kutokuwa makini na Serikali yao “sisi wananchi tumekuwa kama makinda ya ndege yanayoachama mdomo yawekewe chakula,tunaachama midomo watawala wanatuwekewa mdomoni”anasema hiyo kauli aliwahi kuitoa akiwa Kongozi Singida.

Akifafanua kauli yake hiyo alitolea mfano kwenye jimbo analotokea la Musoma Vijijini Ambapo mbunge wake aliwafanyia maendeleo wananchi wake lakini kilipofika kipindi cha uchaguzi mwingine akaja mpiunzani wake yule mbunge akawaambia wananchi mimi nimewasaidia maendeleo na nitaendelea kuwasaidia nichagueni lakini wananchi hawakujali hilo wakamlazimisha kutoa rushwa.

Hali hiyo ilimfanya Butiku amfuate mbunge huyo kumuuliza swala hilo kama alitoa Rushwa akajibiwa kwamba wananchi walimlazimisha wanakwenda hadi nyumbani kwake ikabidi awawekee pesa mezani wagawane, kwa mfano huo anaeleza unajionyesha jinsi maadili yalivyokwisha hata kwa wananchi.

Anasisistiza kuwa viongozi wapo wanaotoa Rushwa ndani ya CCM hakuna anayeweza kupinga hilo, na mtu yeyote akishakuwa kama Kinda atawezaje kuwa Kiongozi au mwanchi mwema? Hata akichaguliwa kuwa Waziri atabaki na ubovu wake huohuo ndio maana Rushwa inadhidi kwa viongozi kutokana na tabaka wanalotokea.

Hali hiyo imekuwepo tangu Uhuru kwani kilikuwa ni kipindi kifupi tu tangu Rais wa Kwanza Mwalimu Nyerere akabidhiwe madaraka na Kuunda Serikali wakati Waziri wake akatuhumiwa kula Rushwa Mwalimu akaamuru atandikwe viboko na kutupwa Jela lakini mwingine aliyehushwa naye akaachwa bila maelezo tangu siku hiyo kulindana kukaanza.

Anasema kuwa tatizo la Rushwa ndani ya Chama cha Mapinduzi na halikuanza leo kwani hata serikali ya awamu ya pili lilikwepo ikafikia hatua ikaundwa tume ya kulichunguza na ikapeleka taarifa kuwa CCM yote inanuka Rushwa, kufuatia taarifa hiyo Rais akaamuru watuhumiwa wakajieleze kwenye mkutano lakini Waziri Mmoja akagoma.

Kutokana na Orodha iliyotajwa Waziri Mkuu wa wakati huo (sasa)Jaji Joseph Sinde Warioba akamshauri Rais Alhassan Mwini avunje Baraza lote kwani kama mawaziri wangejieleza ingekuwa aibu kubwa baraza zima kutuhumiwa kwa Rushwa likaundwa jipya mawaziri saba wakaachwa nje.